IQNA – Sala ya Istisqa (swala ya kuomba mvua) imeswaliwa leo Alhamisi, kufuatia sunnah ya Mtume Muhammad (SAW) ya kuomba rehema ya Mwenyezi Mungu kupitia ibada ya pamoja. Swala hiyo imeswaliwa kufuatia ombi la Mfalme Salman bin Abdulaziz wa Saudi Arabia
Habari ID: 3481508 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/13
IQNA – Wizara ya Hija na Umrah ya Saudi Arabia siku ya Jumapili imezindua rasmi Mkutano na Maonesho ya 5 ya Hajj kwa mwaka 1447 Hijria, yanayoendelea kuanzia tarehe 9 hadi 12 Novemba 2025 katika jiji la Jeddah, chini ya kauli mbiu “Kutoka Makkah Hadi Ulimwenguni.”
Habari ID: 3481495 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/10
IQNA – Nyumba ya Makumbusho ya Sanaa za Kiislamu mjini Jeddah, maarufu kwa jina la Dar al-Funun al-Islamiyyah, imeandaa maonesho ya hati adimu za Qur’ani Tukufu pamoja na kazi za sanaa zinazodhihirisha uhusiano wa kihistoria kati ya imani ya Kiislamu, uzuri wa sanaa, na ustadi wa mikono.
Habari ID: 3481479 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/11/07
IQNA – Mwanazuoni mwenye msimamo wa kihafidhina na aliye katika miaka ya tisini ameteuliwa kuwa kiongozi mkuu wa kidini au Mufti Mkuu nchini Saudi Arabia, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali.
Habari ID: 3481406 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/10/23
IQNA-Katika mwezi wa Rabi al-Awwal 1447 Hijria, Misikiti Miwili Mitakatifu—Msikiti Mkuu wa Makka na Msikiti wa Mtume (SAW) huko Madina, imepokea jumla ya waumini 53,572,983, wakiwemo waumini na mahujaji, kwa mujibu wa taarifa ya Mamlaka ya Huduma za Misikiti Miwili Mitakatifu.
Habari ID: 3481291 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/27
IQNA – Idadi ya safari za ndege zinazowasafirisha waumini wa ibada ya Umrah kutoka Iran kwenda Saudi Arabia imeongezeka tangu mwanzo wa wiki hii.
Habari ID: 3481287 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/26
IQNA – Hatua ya mwisho ya mashindano ya kimataifa ya kuhifadhi Qur’ani Tukufu imeanza Alhamisi katika mji mkuu wa Afrika Kusini, ikiwakutanisha washiriki kutoka nchi 29.
Habari ID: 3481250 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/19
IQNA – Baraza la Mipango na Uratibu kutoka ofisi ya Mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu katika Masuala ya Hija na Ziara, pamoja na Shirika la Hija na Ziara la Iran, wameanza maandalizi ya safari ya Hija ya mwaka ujao.
Habari ID: 3481177 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/09/03
IQNA – Maonyesho ya Kimataifa na Makumbusho ya Maisha ya Mtume Muhammad (SAW) pamoja na Ustaarabu wa Kiislamu yamezinduliwa katika Mnara wa Saa, katika mji mtukufu wa Makkah, siku ya Jumanne.
Habari ID: 3481152 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/29
IQNA – Washiriki wa Mashindano ya 45 ya Kimataifa ya Qur’ani ya Mfalme Abdulaziz wametembelea misikiti ya kihistoria na maeneo ya turathi katika mji wa Madina, kama sehemu ya programu ya kitamaduni iliyoandaliwa na mamlaka za Saudi Arabia.
Habari ID: 3481108 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/19
IQNA – Toleo la 45 la mashindano ya kimataifa ya Qur’ani linaloendelea mjini Makkah limeendelea Jumatatu katika Msikiti Mtukufu (Masjid al Haram), likishuhudia washiriki 18 wakionesha vipaji vyao vya Qur’ani Tukufu.
Habari ID: 3481074 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/12
IQNA – Roboti za kielektroniki zinazoweza kuingiliana na watumiaji zimetumika katika toleo la 45 la Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani yanayofanyika Makkah kwa lengo la kuboresha huduma kwa wageni.
Habari ID: 3481072 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/11
IQNA – Jukwaa la kielimu la Qur’ani kwa ajili ya wasiozungumza Kiarabu linazinduliwa nchini Saudi Arabia.
Habari ID: 3481069 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/11
IQNA – Siku ya pili ya Mashindano ya 45 ya Kimataifa ya Mfalme Abdulaziz ya Kuhifadhi, Kusoma kwa Tajwidi na Kufasiri Qur’ani Tukufu ilishuhudia washiriki 17 kutoka pembe mbalimbali za dunia wakisoma mbele ya hadhira katika Msikiti Mtukufu wa Makkah.
Habari ID: 3481068 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/08/11
IQNA – Huduma za Hija kwa Waislamu wa Afrika Kusini sasa zitawekwa chini ya usimamizi wa Baraza la Hija na Umra la Afrika Kusini (SAHUC).
Habari ID: 3480961 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/18
IQNA – Taasisi ya Mfalme Abdulaziz nchini Saudi Arabia imechapisha kitabu kipya kwa lugha ya Kiarabu kinachofuatilia historia ya maendeleo ya zana zilizotumika kuandika Qur’ani Tukufu.
Habari ID: 3480955 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/07/16
IQNA – Maombi ya visa za Umrah yameanza tena rasmi siku ya leo Jumanne, tarehe 10 Juni, hivyo kuwapa fursa waumini kutoka mataifa mbalimbali kuanza maandalizi ya safari tukufu kuelekea miji mitakatifu ya Makkah na Madinah kwa ajili ya Hija ndogo ya Umrah.
Habari ID: 3480820 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/10
IQNA – Shirika la Hija la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limetunukiwa Tuzo ya Labaytum kwa ubora katika Huduma kwa Mahujaji.
Habari ID: 3480810 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/09
IQNA – Takriban Mahujaji milioni 1.7 wamekusanyika katika ardhi tukufu ya Saudi Arabia kumaliza ibada muhimu za Hija, ambazo zilihitimishwa kwa ibada ya kutupa mawe katika eneo la Mina na kuzunguka Kaaba kwa mara ya mwisho (Tawafu ya kuaga) katika Msikiti Mtukufu wa Makkah.
Habari ID: 3480804 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/06/08
IQNA – Zaidi ya Waislamu milioni moja kutoka nje ya Saudi Arabia wamewasili katika ufalme huo kwa ajili ya kushiriki katika ibada ya Hija ya kila mwaka, mamlaka husika zimetangaza siku ya Jumatatu.
Habari ID: 3480749 Tarehe ya kuchapishwa : 2025/05/27